Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Dunia ina vituko vyake mtu wangu, na kwa wenzetu wa Marekani wakati mwengine vituko huzua madhara makubwa.

Nimekutana na hii moja inayomhusu Dontavian Eagle McCree mwenye miaka 19 aliyeachiwa jukumu la kukaa na mtoto wa dada yake wakati yeye akiwa kazini.

Siku moja wakati akiwa nyumbani na mtoto wa dada yake, Dontavian aliamua kumpatia mtoto huyo wa miezi 10 pombe, akachanganya pombe kwenye maziwa ya mtoto na kumnywesha.

Dontavian Eagle McCree,19.

Siku chache baadae mtoto alianza kuumwa na baada ya mama yake kugundua aliamua kumpeleka mtoto hospitali na ndipo alipogundua kuwa mtoto alinyweshwa pombe.

Dontavian amekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na thamani ya dhamana yake ni dola 15,000 ambayo ni sawa na Mil.30 za Kitanzania. Hali ya mtoto sio nzuri kabisa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top