March 17, 2025 03:25:52 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.

Kwa mujibu wa gazeti  la Risasi, Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao walifika na kukaa meza nyingine.

Habari zinadai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt tangu ajifungue.
 
Inadaiwa kuwa baada ya Aunt kumaliza kula Ice Cream na kundi lake, waliinuka na kuondoka zao na kumuacha Wema na marafiki zake.
 
Alipotafutwa  Aunt ili aweze kuzungumzia kitendo hicho na bifu laolisema;
 
“Jamani unajua kila mtu alienda kwa ajili ya kazi zake na ndiyo kama tulivyokutana kila mmoja alikuwa yupo na taratibu zake, sioni kama ni bifu, sina comment,” .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
22 Jul 2015

Post a Comment

 
Top