Kikao cha Bunge kilianza kama kawaida leo July 02 2015, baada ya kipindi cha maswali na majibu yaliyoulizwa kwa Mawaziri, Mbunge John Mnyika akaomba mwongozo.
βTumekabidhiwa orodha ya shughuli za leo.. kimsingi imekiuka kanuni, uamuzi wa kuileta hii miswada mitatu kwa pamoja kama hati ya dharura umekiuka kabisa msingi wa makubaliano ya kwenye Semina ambapo Wabunge kwa kauli moja tulikataa Miswada hii isiletwe kwa hati ya dharuraβ
βNaomba Mwongozo, hili jambo linahitaji majibu sasaβ >>> Mbunge John Mnyika.
Spika Makinda akaanza kutoa ufafanuzi kuhusu hiyo ishu >>> βToa kwanza maneno ya kuniamrisha mimi cha kufanyaβ¦ Hakuna mtu anayeweza kuniamrishaβ >>> Anne Makinda.
Spika akaendelea >>> βTumefanya mara nyingi sana wala sio leo tu, hakuna kanuni iliyovunjwa na sio mara ya kwanza kujadili kitu kinachofanana kwa pamojaβ>>> Spika Anne Makinda.
Hakukuwa na suluhu ya hilo, Wabunge wa Upinzani wakagomea Mjadala huo kuendelea ikabidi Kikao cha Bunge kiahirishwe saa nne asubuhi. Angalia Video Hapa:
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment