March 19, 2025 05:37:50 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge wa viti maalumu Singida,amesema anafurahishwa na kitendo cha mashabiki wake kumwigiza sauti akiwa bungeni kwa  kuwa wameonyesha kumkubali kabla hajafika β€˜Mjengoni’.

Alisema sauti hiyo inayomuigiza alitumiwa kupitia simu yake na haikumkwaza zaidi ya kufurahia  kwamba watu wengi wanakubali awe bungeni.
β€œNafurahi kwa kuwa wengi wameshanipeleka bungeni wakati mimi ndiyo kwanza nipo katika harakati  za kuomba kuchaguliwa kupitia umoja wa wanawake Singida , lakini nafurahia kwa kuwa inaonyesha wengi wananikubali,  ila nikipitishwa kuwawakilisha wana Singida bungeni sitaongea kama walivyonirekodi katika sauti hiyo,” alisema Wema kwa furaha.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
23 Jun 2015

Post a Comment

 
Top