Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephati Gwajima amesema kwamba mwananchi  au mwanasiasa  yeyote asiyempenda Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akale limao

Askofu Gwajima alisema hayo juzi  mara baada ya Edward Lowassa kumaliza hatuba yake wakati akitangaza  nia ya kutaka kugombea  urais katika uchaguzi mkuukwa  tiketi  ya  Chama cha Mapinduzi, CCM.

Kabla ya kumaliza hotuba yake wananchi walimshinikiza Edward Lowassa amsimamishe Askofu Gwajima  ndipo Lowassa alimuita na kumpa maiki aongee na wananchi waliofurika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha.

Askofu Gwajima  alianza kwa kuomba mwenyezi Mungu aibariki safari ya Matumaini ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa na mwisho kabisa kuwapa mjumbe mzito wananchi kuwa mwenye Chuki na Lowassa akale limao.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top