Home
»
Idris Sultan
»
wema sepetu
» Wema Sepetu na Idris Sultan Nusura Wazichape Kavukavu Kisa Wivu wa Mapenzi.
Malkia anayemiliki Kampuni ya Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu na Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15, Idris Sultan ambao wamekuwa marafiki wakubwa katika siku za hivi karibuni, nusu wazichape kavukavu baada ya kupishana kauli huku wivu wa kimapenzi ukitajwa.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar ambapo kwa pamoja walikuwa wamehudhuria sherehe ya utoaji Tuzo za Watu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tafrani ya wawili hao kutaka kukunjana ilitokea baada ya kumalizika kwa shuguli hiyo ambapo Idris alimpora Wema tuzo yake aliyoshinda na kwenda nayo kwenye gari lake.
Ugomvi huo ulipamba moto na kusababisha watu waliokuwa wakiwashuhudia kutaharuki ambapo Wema alikwenda kwenye gari lake lililokuwa likiendeshwa na Petit Man lakini Idris alimfuata akionekana kumuonea wivu na kumtaka apande gari lake waondoka jambo ambalo Wema alilitolea nje na kumfungia kioo.
Baada ya kuona Wema amemtolea nje, Idris alikwenda kwenye gari lake na kuliegesha mbele ya gari la Wema ‘kum-block’ ili asiondoke ambapo alishuka na kumwambia Petit Man ahakikishe anamfuata kwa nyuma jambo ambalo Petit Man alishindwa kulitekeleza baada ya Wema kukataa.
Baada ya kushuhudia vurugu hizo, mwanahabari wetu alimfuata Wema ili kujua kilichotokea ambapo mwanadada huyo alisema kuwa haelewi ni kitu gani ambacho kilimkuta Idris siku hiyo maana kama angekuwa anakunywa pombe, angesema labda alizidiwa lakini kwa kilichotokea hadi leo hajui ni kipi kilimkuta.
“Yaani hata sielewi Idris alifikwa na nini maana amefanya mambo ya ajabu sana na mara ya kwanza nilijua utani lakini nilimshangaa zaidi baada ya kukomaa hadi kufikia hatua ya kuni-block na gari lake huku akitaka niondoke naye wakati kila mtu alikwenda pale kimpango wake.
“Mimi nadhani kuna utoto fulani bado anao na unamsumbua,” alisema Wema lakini Idris hakupatikana kusema chochote.
Credit: Gpl
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Wema Sepetu ampigia magoti Idris Sultan22 Aug 20160
Uhusiano wa Wema Sepetu na Idris Sultan unaanza kutukumbusha ule wa Chris Brown na Karrueche Tr...Read more ?
- VIDEO: Mama Wema Aeleza Beef yake na Man Fongo Kisa……..09 Sep 20160
NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa ...Read more ?
- Wema Sepetu: Niacheni jamani Nimechoka03 Aug 20160
Wema Sepetu Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali k...Read more ?
- Idris Sultan Amtundika Mimba Wema Sepetu25 Jan 20160
Mshindi wa Big Brother Afrika, Idris Sultan amepasua jipu kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu...Read more ?
- Kipindupindu Chanyemelea Nyumbani Kwa Wema Sepetu28 Aug 20150
Mrembo Wema Sepetu Taarifa za ugonjwa wa kipindupindu zimebadili mfumo wa maisha ya watu wengi i...Read more ?
- Wema Sepetu na Lowassa ni 'Paka na Chui'......Atoa ONYO Kali Kwa Team Wema11 Aug 20150
Kama unamfatilia Wema Sepetu kwenye mitandao yake ya kijamii jana kupitia mtandao wa Instagram a...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment