March 15, 2025 01:02:32 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
UTATA umeibuka kutoka Pambano la Karne baina ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililofanyika juzi ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani.

Karatasi ya kuandika matokeo raundi kwa raundi ya majaji wote watatu, Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti inaonyesha bondia aliyekuwa kona nyekundu, Pacquiao ndiye aliyeshinda pambano, wakati mtangazaji 'MC' wa pambano akamtangaza bondia wa kona ya bluu, Mayweather ndiye mshindi.

Inaonekana kama majaji walijichanganya katika kutumia karatasi hizo na pointi za Mmarekani, Mayweather 'Mtu Pesa' wakizihamishia kwa Mfilipino, Pacquiao, lakini kwa nini iwe kwa majaji wote watatu?

Hii inazidi kuzua shaka kwamba inawezekana Mayweather alipewa ushindi kimakosa bali kwa mujibu wa karatasi za majaji mshindi ni Pac Man aliyekuwa anatokea kona nyekundu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
05 May 2015

Post a Comment

 
Top