Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo sehemu nyeti.
 
Kwa mujibu wa chanzo ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.

“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
 
“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
 
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
07 May 2015

Post a Comment

 
Top