Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
IMG_4680.JPG
Samatta anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji watanzania wanaoingiza fedha nyingi kupitia soka – akiripotiwa kulipwa mshahara usiopungua $8000 kwa mwezi bila kuongeza marupurupu.

Mmoja ya wachezaji wa kitanzania wenye mafanikio katika soka nje ya mipaka ya Tanzania, Mbwana Samatta leo asubuhi ameposti picha ya gari lake jipya analotumia akiwa nchini Tanzania.
Gari aliloposti Samatta ni Range Rover lenye rangi ya damu ya mzee ambalo lina namba za usajili za Tanzania na linakua gari la pili la thamani ambalo Samatta ameliweka hadharani baada ya mwaka 2013 kulionyesha gari lake aina ya Chrysler Crossfire ambalo lilikuwa na thamani ya takribani millioni 50 za kitanzania. 
Samatta alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba SC kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa kipindi hicho ya $100,000.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
26 May 2015

Post a Comment

 
Top