Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
----
Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu
Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza
kujiuzulu nafasu hiyo Jioni hii katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya
CCM,Mjini Dodoma
Akithibiths tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi
,Naoe Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa
CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya
CCM katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu
Mwigulu alishakuwa amemwambia nia hiyo Mwenyekiti wa
Chama Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa leo katika kikao
ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya
wajumbe wa NEC hii leo'..amesema Nape
Nape amesema kufwatia uamuzi wa mwigulu Mwenyekiti wa
Chama Rais Jakaya Kikwete katika nafasi yake amemteua Msaidizi wake maswala ya
siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kumteua kuwa Naibu
Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment