Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Musa mateja
Jino kwa jino! Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba.

Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo?

Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia kuwa ninatoka  au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii.

“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na kuongeza:

Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 May 2015

Post a Comment

 
Top