Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
JESHI la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Gerald Paulo (34) kwa kosa la kumpiga binti yake, Anisia Gerald (14), sehemu mbalimbali za mwili wake na kumyonga kwa kutumia kanga.

Akizungumzia tukio hilo mjini hapa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu katika Kijiji cha Rugazi Kyaitoke kisha alichimba kaburi nyuma ya nyumba yake na kumzika.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa jirani ya Paulo kuwa ameua binti yake na walipofuatilia walibaini ni kweli.

Alisema baada ya polisi kufukua kaburi hilo walikuta mwili wa binti huyo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kipande cha kanga shingoni.

Kwa taarifa nilizonazo, Gerald si mara ya kwanza kufanya mauaji kama hayo, maana miaka mitano iliyopita aliwahi kuua mtu na kukimbilia Karagwe kwa jinsi hiyo hiyo, kwa tukio hili lazima sheria zichukue mkondo wake,” alisema Mwaibambe.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top