Home
»
CCM
» Lowassa Na Wenzake Sasa Wako Huru....Adhabu Yao Imekwisha LEO......Taarifa Kamili Iko Hapa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa Sekretarieti kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma leo tarehe 22 Mei 2015.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi kisichopungua miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye
Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika Chama.
Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya wagombea utakapofika.
Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.
Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
22/05/2015
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Kikwete Atoa Dongo "Wapo Watu Walidhani CCM ingekufa na Walishajiandaa na Salamu za Rambirambi"22 Jul 20160
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amekata mzizi wa f...Read more ?
- Makapi Aliyosema Katibu Mkuu wa CCM Mh. Kinana Haya Hapa06 Aug 20150
“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi ...Read more ?
- Kikwete: CCM Si Chama Cha Mchezo.......Wapinzani Watakiona cha Mtema Kuni Mwaka Huu05 Aug 20150
MWENYEKITI wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amesema chama hicho sio chama cha mchezo na kuvi...Read more ?
- Vikao Vyote vya CCM Kufanyika Leo Na Majina ya 5 Bora na 3 Bora Yatajulikana leo10 Jul 20150
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema, leo hii majina ...Read more ?
- Moshi Mweusi Watanda CCM.......Rais Kikwete Apangua Ratiba ya Vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati Kuu, Kingunge Amvaa Kinana10 Jul 20150
WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akipangua ratiba ya vikao m...Read more ?
- Mangula Ataja Vigezo 13 Vya Mgombea Urais wa CCM09 Jun 20150
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula amesema vigezo 13, vitatumika kuwa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment