March 18, 2025 06:21:21 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Idara ya ujasusi ya Korea Kusini imesema kuwa waziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.

Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alikutana na mauti yake baada ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi Aprili.
Bwana Hyon anasemekana kuwa alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na rais Kim jambo lililomuudhi sana kiongozi huyo wa kiimla.
Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa serikali ya Korea Kaskazini.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa
Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa korea kaskazini kuamrisha kuuawa kwa kiongozi mkuu serikalini ilikuwa ni mwaka wa 2013 alipoamrisha ami wake
Chang Song-thaek - kukamatwa na kutiwa kitanzi.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa mbele ya umma.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 May 2015

Post a Comment

 
Top