Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Manchester United 1-1 Arsenal: Tyler Blackett own goal hands Gunners a precious point
Hatimaye ligi kuu ya England inaelekea kufikia tamati huku vita ya vilabu vya Man City, Arsenal na Man United ya kujihakikishia nafasi ya pili na ya tatu ikiwa nayo inaelekea mwishoni.
Mapema hivi leo City walijihakikishia kumaliza ndani ya top 3 baada ya kuwafunga Swansea 4-2 na kuziacha United na Arsenal wakipambana kuwania nafasi mojawapo kwenye top 3.
Vilabu hivyo muda mfupi uliopita vilikuwa vinatoana jasho katika dimba la Old Trafford na matokeo ya mchezo yameipa Arsenal uhakika wa kumaliza kwenye aidha nafasi ya pili au tatu kwenye Barclays Premier League.
Mechi hiyo imemalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1 kwa United na Arsenal.
Ander Hererra alifunga goli zuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao kilikuwa kimetawaliwa na United kabla ya Arsenal kurudi kipindi cha pili na kusawazisha goli hilo kupitia Tyler Blackett aliyejifunga.
 
Kwa matokeo hayo Arsenal ambao wana mechi mbili mkononi wanaendekea kushika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 71 na United wana mchezo mmoja wakiwa na pointi 69.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top