KESI ya kumtesa mfanyakazi wa ndani inayomkabili mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige (42), imeahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jana kutokana na mshtakiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumkata kwa mapanga.
Shauri hilo litakuja tena Juni 16, mwaka huu endapo hali ya mshtakiwa ikiendelea vizuri.
Mbele ya Hakimu Yohana Yongolo, Wakili upande wa Jamhuri ulidai kwamba shauri hilo lipo mbele ya mahakama hiyo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa ushahidi upande wa mlalamikaji.
Mdhamini wa pili wa mshtakiwa Chausiku Maige, aliiambia mahakama hiyo kwamba Amina ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa alivamiwa na watu wasiojulikana ambapo tukio hilo lilitokea nyumbani kwake Mei 7, mwaka huu.
“Mheshimiwa mtuhumiwa kwa sasa yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Taasisi ya Mifupa (MOI), akiendelea na matibabu baada ya tukio hilo lililotokea nyumbani kwake alfajiri wakati akitoka ndani kuelekea kazini.
“Tulitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Osterbay kisha tulipewa RB/7647/2015. Amina amepata majeraha makubwa sehemu za mkononi pamoja na kichwani,” alidai Chausiku.
Hakimu alimhoji mtuhumiwa huyo kama eneo analoishi mtuhumiwa huyo ana uhasama na jirani zake, ambapo shahidi huyo alijibu kuwa hajui kwa kuwa haishi naye karibu.
Amina Maige kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo Juni 13, mwaka jana akikabiliwa na tuhuma za kumchoma pasi na kumng’ata mfanyakazi wake wa ndani, Yusta Kashinde (20) hali iliyosababisha maumivu makali mwilini.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment