March 25, 2025 07:45:05 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwa anashangazwa na viongozi wa CHADEMA kuhoji anakotoa fedha za kugharamia mikutano na ziara za ACT-Wazalendo pamoja na kujinadi kwa wananchi.


Zitto amewajibu jibu jepesi kwa kusema “CHADEMA walianza bila ruzuku, waulizeni fedha za ziara zao za kuzunguka kwa helkopta nchi nzima walizitoa wapi? Kule walikopita ndiko na mimi ninakopita huku na huko” alisema huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha

Alifafanua kuwa fedha za chama chake wanazofanyia ziara zinatokana na michango mbalimbali ya watu wenye nia njema na chama hicho, Zitto pia aliwataka wananchi wa Mwanza kuchuja na kuchagua uzalendo. “Chujeni mtu mwenye hoja twendeni tukaijenge nchi”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
23 Apr 2015

Post a Comment

 
Top