March 16, 2025 02:00:07 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
leooo
Yanga Bingwa 2014/2015!! Hizi ni baadhi ya headlines kwenye kurasa za michezo.. haikumaanisha kwamba matokeo ya mwisho yalikuwa yameamua hvyo, ila wanspoti walipiga hesabu ya pointi ambazo yatari YANGA walikuwa wamejikusanyia mpaka mechi yao ya mwisho, hii ya leo ambayo Yanga wamekutana na Polisi Morogoro tayari imetoa matokeo.

Yanga imefikisha jumla ya pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi kuu msimu huu, kwa matokeo hayo basi Yanga wanakuwa mabingwa wa Ligi hiyo.
Mechi hiyo kati ya Yanga na Polisi Moro ilikuwa ikipigwa katika Uwanja wa Taifa Dar.. mechi imekamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa goli 4-1.
Hamis Tambwe leo aliweza kuing’arisha Yanga baada ya kupachika magoli matatu ambapo goli la kwanza alifunga dakika ya 40 kufuatia krosi ya Saimon Msuvagoli la pili alilifunga dakika ya 53 na goli la mwisho alifunga baada ya kupokea cross kutoka kwa Mrisho Ngassa.
Msuva alikamilisha idadi ya mabao kwa kupiga bao la nne ambapo baadae dakika ya 83 Polisi walishinda bao la kufutia machozi kupitia kwa Bantu Admini aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18.
Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kukamilika mwisho wa wiki katika mechi za kukamilisha ratiba ya ligi hiyo kwa msimu huu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
28 Apr 2015

Post a Comment

 
Top