Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kweli mitandao ya kijamii ina kazi. Ukiwa na moyo mwepesi mitandao hii inaweza kuwa sio wazo zuri sana kwako.
Leo kupitia mtandao, mwanadada Aunty Ezekiel amepata na jambo ambalo kwa upande wetu tunaona si la kiungwana hata kidogo baada ya jamaa mmoja kuandika maneno yasio ya kibinadamu hata kidogo kwenye picha moja aliyoiweka mwanadada huyo ambaye ni mjamzito .

Aunty Ezekiel aliweka picha yake akiwa na Wema Sepetu ambaye hapo jana aliamua kufungua juu ya tatizo lake linalomsumbua la kutoweza kushika ujauzito, na baada ya kuweka picha hiyo ndipo alipopatwa na dhahama hiyo baada ya jamaa huyo kuandika kuwa anatamani aunty Ezekiel akijifungua tu afe pamoja na mtoto wake huyo, jambo ambalo si la kibinadamu kabisa kumuombea mtanzania mwenzako

Yani ukijifungua naomba ufe na mimba yako maana utakachozikaa kimelaaniwa” Hayo ndio yalikuwa maneno ya kijana huyo.

Baada ya kauli hiyo Aunty Ezekiel aliamua kuandika haya yafuatayo…

“Ukiacha yote ktk Maisha naamini Duniani tunapita na kila mmoja wetu yupo ktk safari ugumu ni kutangulia na Mwenyezi Mungu si wa kwako wala wakwang na ndio mana kila mmoja anatimiziwa haja zake kwa nafasi yake Nataka nikwambie tuu ww kaka uliyeandika maneno hayo kwang leo kuwa ww ni wa Mwenyezi Mungu pia dua lako linawezekana kusikilizwa na likasikilizwa haraka couse wala haupo peke yako ila ww ndie pekee uliepata ujasiri wa kuandika wengine watakuwa wanaomba kwa chini ila wote tumuombae hayo ni huyo huyo mmoja hvyo bac tumuachie yy Inshaalah ndio anajua mwisho wa kila mmoja wetu.Furaha ni ya zamu utakapokuwa unafurahia Umauti wang Familia yang itakuwa ikilia kwa hilo na ifikapo kwako ww unaeniombea hilo kila kukicha ni hvyohvyo pia kwa familia yako.Hvyo nina Aman yakutosha tu kwakuwa mm ni wakwake pia Sikujiumba.WHN JESUS SAY YES NO BD CAN SAY NO....love u all.....”

Pole sana Aunty Ezekiel. Tunakuombe ujifungue salama.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top