March 18, 2025 06:34:02 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
7__eden_hazard___wallpaper_by_aa_designs-d6qocihLigi kuu ya England inakaribia ukingoni, na tayari timu mbalimbali zimeshapata taswira kamili ya nini zimepanda kwa msimu mzima wa ligi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.
Chelsea bado ina matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na wiki ijayo inaweza kutangaza ubingwa endapo itaifunga Crystal Palace baada ya jana kutoka sare ya 0-0 na vibonde wa Arsenal.. Mpaka sasa Chelsea ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi zake 77 mkononi.
hazard
Stori ambayo ipo kwenye headlines kwa sasa ni kuhusu kiungo wa ChelseaEden Hazard ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha wachezaji wa kulipwa England, PFA.
players
Mchezaji huyo nyota raia wa Ubelgiji ameifungia Chelsea jumla ya mabao 18 akiiwezesha kutwaa taji la kombe la ligi maarufu Capital One pamoja na kuwa mmoja ya wapambanaji waliosukuma jahazi la Chelsea kuelekea kwenye jukwaa la ubingwa kwa mara nyingine tangu mwaka 2010.
Hazard amekabidhiwa zawadi hiyo katika hotel ya Grosvenor Hotel iliyopo London.
Kwa upande wa mwanasoka bora chipukizi mshambuliaji hatari wa SpursHarry Kanealifanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kuwapiku kipa David De Gea wa Man Unitedna Raheem Sterling wa Liverpool.
Tuzo ya heshima ilikwenda na Steven Gerrard na Frank Lampard kutokana na mchango wao mkubwa kwenye ligi kuu ya England.
_82583402_edenhazard_1
Hii ni record ya Hazard
Baada ya Hazard kutangazwa mshindi, staa wa soka Allan Shearer amesema ubora waHazard anafaa kuwa mchezaji bora wa dunia.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
27 Apr 2015

Post a Comment

 
Top