Siku chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutangaza kujiunga na chama cha ACT-Tanzania, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amemtaka kujenga upinzani wa kweli kwa ajili ya kujenga nchi na si kubomoa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Nape alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo upya katika ulingo wa siasa.
Alisema kinachotakiwa ni upinzani wenye lengo la kujenga na Zitto akitaka heshima aachane na siasa za Chadema zenye lengo la kuvuruga.
Hata hivyo, alisema hawawezi kuwa na mfumo wa vyama vingi vyenye lengo la kubomoa, hivyo ajenge upinzani wa kweli wa kuijenga nchi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment