March 20, 2025 09:44:51 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
KATIKA hali ya kustaajabisha, Mtangazaji wa Kipindi cha The Mboni Show kinachoruka katika Runinga ya TBC1, Mboni Masimba alipigwa na butwaa baada ya kuzawadiwa mbuzi aliyefungwa kanga kwenye sherehe ya Maulid.
Tukio hilo la aina yake lilijiri juzikati nyumbani kwa mtangazaji huyo Masaki jijini Dar ambapo Mboni alipokuwa akimfanyia sherehe hiyo mwanaye, Prince Milan aliyekuwa akitimiza siku arobaini tangu kuzaliwa kwake.
Tofauti na ilivyozoeleka katika sherehe hiyo watu kupeana zawadi za nguo na vifaa vya mtoto, mashosti zake akiwemo Jestina George, Hawa Mkamba, Shamimu ‘Zeze’, Nargis Mohammed na wengineo, walimpa zawadi za kawaida lakini MC Gladys Chiduo  ‘Zipompapompa’ aliwashangaza watu kwa kumpatia zawadi ya mbuzi aliyemfunga kanga kiunoni.

“Mh! Hii leo mpya, tumezoea wenye sherehe kama hizi watu tunatoa vifaa vya mtoto leo ameletwa mbuzi amefungwa kanga, leo kazi ipo,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa sherehe hiyo.Zipompapompa alipoulizwa sababu za kuibuka kwenye sherehe hiyo na mbuzi aliyevishwa kanga, alifafanua hivi:
 
“Hii ni kanga mpya kabisa tumemfunga mbuzi kama mkaja, iwapo mbuzi atachinjwa mama mtoto atachukua kanga yake kama mama mzazi anapopewa mkaja wakati mwanaye anaolewa, mbuzi itakuwa ni supu kwa mzazi.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
23 Apr 2015

Post a Comment

 
Top