Asubuhi ya leo imeripotiwa stori ya Askari Polisi wakiwa na silaha kuizunguka nyumba yake, Mbezi Salasala DAR.. waumini wake, waandishi wa habari pamoja na watu wengine walikuwa pembeni pia, kuangalia kinachoendelea.
Muda mfupi baadae imeripotiwa kwamba Askofu huyo alienda Kituo cha Polisi Centre lakini haikuchukua muda mrefu akatolewa na kupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu DAR..
Taarifa kutoka Mahakamani zinaarifu kuwa Gwajima amepata dhamana na atarudi mahakamani hapo Mei 4, 2015.
Josephat Gwajima ameshitakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza silaha.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment