Siku moja baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la mbunge wa Kigoma kaskazini Mh Zitto Kabwe kujadiliwa na vikao vya CHADEMA kuhusu hatma ya uanachama wake na kutakiwa kulipa gharama za kesi hiyo, mbunge huyo amedai kuzisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari lakini hana taarifa rasmi.
Hayo ndio yalikuwa majibu ya awali ya mbunge huyo wa Kigoma kaskazini alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wake haraka , mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, Mh Tundu Lisu alizungumza na vyombo vya habari kuhusu Chadema kutomtambua Mh Zitto kama mwanachama wa chama hicho.
Ili kusikia kauli ya Mh Zitto kuhusu suala hilo Mpekuzi ilifika katika ofisi ndogo za bunge zilizoko jijini Dar es Salaam na kumshuhudia Mh Zitto akiongoza vikao vya kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu ya mashirika ya uma PAC ambapo baada ya kumalizika kwa kikao hicho,Zitto alizungumzia maamuzi hayo ya mahakama na Chadema baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari.
"Taarifa hizo hata mimi nimezisikia mitandaoni na katika vyombo vya habari.Sina taarifa rasmi ya kuvuliwa uanachama na nipo kazini kama mnavyoniona.....
"Hata kama chama kingekuwa kimeamua hivyo, bado kuna taratibu za kufuata. Wanatakiwa kumwandikia barua spika wa Bunge ili ajiridhishe juu ya maamuzi hayo na kisha awajibu.
"Pia, maamuzi ya kumvua ubunge au uanachama mtu flani hayafanywi na mtu mmoja, ni lazima kikao halali cha chama kikae na kuamua hivyo." Alisema Zitto Kabwe

Aidha kutokana na madai hayo, Mh Zitto amesema kwa kuwa hana taarifa rasmi ijumaa ya wiki hii atakwenda jimboni kwake kuzungumza na wananchi wa jimbo lake kama mbunge na kisha jumanne ya wiki ijayo atahudhuria vikao vya bunge kama kawaida na kuongeza kuwa tukio hilo linamkomaza kisiasa na kwamba siasa zake ni zakujadili masuala na si watu kama walivyo baadhi ya wanasiasa wenzake.
"Sina haja ya kujibizana nao, sijalelewa hivyo kisiasa.Ijumaa hii ntaenda jimboni kwangu kuzungumza na wananchi kama mbunge halali". Amesema Zitto Kabwe.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment