March 18, 2025 07:05:13 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 82 kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo mkali kusababisha mafuriko katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu 3,500  bila makazi katika kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya mifugo ikisombwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika kata ya Mwakata kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
Tanzama picha hapa chini:

Miili ya watu 7 wa familia moja waliokufa katika tukio hilo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
04 Mar 2015

Post a Comment

 
Top