Timu ya Sunderland imemtimua kocha wake Gus Poyet, hii ni kutokana na taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Kocha
huyo mwenye uraia wa Uruguay ambaye amedumu kwa muda wa miezi 18 tu
kwenye klabu hiyo, ametimuliwa kutokana na timu yake kutokuwa na matokeo
ya kuridhisha hasa mara baada ya kupokea kipigo cha magoli 4-0 kutoka
kwa Aston Villa juma lililopita katika uwanja wao wa nyumbani.
Siku ya kipigo hicho kuna baadhi ya washabiki wenye hasira walidiriki kutaka kumpiga baada ya kukasirishwa na matokeo hayo.
Ikumbukwe
tu Sunderland mwanzoni mwa msimu huu walishawahi kufumuliwa vibaya na
Southampton nyumbani kwao hapo hapo baada ya kukubali kipigo cha magoli
7-0.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment