Tukio lililosikika leo kwenye Hekaheka ni
ishu ya baba mmoja kumuunguza mtoto wa jirani kama njia ya kuulipiza
kisasi cha mtoto wake kuunguzwa kwa bahati mbaya wakati wakicheza na
wenzake.
Mtoto huyo amesema alikuwa anatoka nje
akiwa amebeba sufuria la moto, mtoto mmoja akatokea akiwa anakimbia na
kugongana naye, mtoto huyo akaungua kwa bahati mbaya kichwani.
Baadae watoto walikuwa uwanjani
wanacheza, baba wa mtoto aliyeunguzwa alimuita mtoto ambaye alimuunguza
mwanae na kwenda naye nyumbani kwake, akaweka kisu jikoni na kumchoma
nacho sehemu mbalimbali mwilini kama kulipiza kisasi.
Majirani baada ya kugundua tukio hilo
waliamua kwenda kushtaki Serikali za mitaa kutokana na mama ambaye mtoto
wake amechomwa kulipiza kisasi kuogopa kutoa taarifa akihofia kufukuzwa
kwenye nyumba hiyo aliyopangishwa na baba ambaye kamchoma mwanae.
Polisi walifika eneo hilo na kumkamata mtuhumiwa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment