Itakumbukwa kwamba, baada ya kifo cha Kanumba, mama yake mzazi, Flora Mtegoa ndiye aliyeshika jukumu la kusimamia mali za marehemu mtoto wake (alikuwa na haki).
Habari ambazo zimeandikwa na gazeti hilo zilidai kwamba, mpangaji mwingine aliikodisha ofisi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini hivi karibuni mtu huyo amefariki dunia.Msikilize shuhuda: “Kuna jamaa alipanga kwenye ofisi iliyokuwa ya Kanumba mara tu baada ya mama Kanumba kuondoka vitu kwa kushindwa kulipia mkataba mpya.
Kifo cha mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, kinaunganishwa na tukio lilitokea mwaka juzi baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 7, mwaka 2012.Mara baada ya Kanumba kufariki dunia ghafla, mwanamke mmoja alikwenda kupanga nyumba ile aliyokuwa akiishi marehemu iliyopo Sinza, Dar, naye alifariki dunia ghafla.
Wakati wa tukio hilo, wanahabari wa gazeti hilo walifika nyumbani kwa mwigizaji huyo ambapo walizungumza na majirani wakaelezea juu ya uwepo wa tukio hilo.Walisema japo hawaamini juu ya imani za masuala ya mzimu wa marehemu lakini kitendo cha mwanamke huyo kufariki dunia muda mfupi baada ya Kanumba kufa kiliwafanya washtuke na kuamini kwamba huenda ni mzimu wa Kanumba ndiyo ulichukua roho ya mpangaji huyo.
Hata hivyo, baadhi ya watu wengine pia walisema yao wakidai kwamba, wanaamini kifo cha mwanamke huyo ni cha kawaida kama ilivyo kwa vifo vingine.“Kama siku za Kanumba zilivyokuwa zimewadia na huyo mpangaji pia siku zake zilikuwa zimefika ndiyo maana amefariki dunia,” alisema mmoja wa majirani.
Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Sumali (76), mkazi wa Mabibo-Relini, Dar akizungumza na gazeti hili kuhusu mazingira ya vifo hivyo, alisema:“Ipo mizimu ya hivyo. Mtu akifa, wa kwanza kuhamia kwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu naye anakufa. Lakini si kwamba nyumba ndiyo ina mizimu. Kama hivyo vifo vimetokea kweli basi na mzimu wa Kanumba umeshaondoka.”
Baada ya kuzipata habari hizo, mwanahabari wa gazeti hilo alimvutia waya mama Kanumba kutaka kujua kama anajua lolote juu ya marehemu mtoto wake kuacha mzimu ambao unahusishwa na vifo hivyo ambapo alikiri kusikia taarifa za kifo cha jamaa aliyepanga kwenye ofisi za Kanumba lakini akasema hata yeye hajui sababu za kifo chake.
Post a Comment
Post a Comment