Siku chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando kufichua njama za Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi kupanga mipango ya kumuua katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye Mlinzi huyo ameibuka na kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho kikuu cha upinzani nchini..
Akifichua siri hiyo leo mchana Jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari, Kangezi amesema amesikitishwa sana na madai ya uongo yanayoenezwa na viongozi wa CHADEMA huku wakificha ukweli wa Mambo kwani ukweli wa yeye kuzushiwa uongo huo unatokana na kuwa na mahusiano na Mke wa Dr. Slaa .
“Nawashangaa sana hawa Viongozi wa Chadema wanaosema mimi ni nimehusika katika mipango ya kumuua Dr. Slaa. Wanaficha ukweli tu kwani sababu ya kuzushiwa uongo huu inatokana na mimi kuwa na mahusiano mabaya na Mke wa Slaa...
"Nilipoenda kumwabia Slaa, alisema niende nikamalizane na mke wake lakini ukweli ni kuwa mambo hayakwenda vizuri, mke wake hakunielewa , ndipo Slaa akapeleka sakata hilo kwenye uongozi wa juu” amesema kagenzi na kuongeza:
"Nilipoenda kumwabia Slaa, alisema niende nikamalizane na mke wake lakini ukweli ni kuwa mambo hayakwenda vizuri, mke wake hakunielewa , ndipo Slaa akapeleka sakata hilo kwenye uongozi wa juu” amesema kagenzi na kuongeza:
"Baada ya Dr. Slaa kupeleka ugomvi huo kwenye ngazi za juu,juzi wakati naenda ofisini nilikamatwa na kupelekwa chumba cha mateso kinacho milikiwa na Chama hicho"
Bwana Kagenzi ameendeleo kusema kuwa hata madai wanayodai kwamba anauhusiano wa karibu na usalama wa Taifa pamoja na Vigogo wa CCM ni ya uongo.
“Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uongo wa hali ya juu na wanataka kunichafua kwa jamii tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.
“Mimi nimekuwa mlinzi wa Dr. slaa kwa muda wa miaka mingi sana ,tena nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua ? Huo ni unafiki” amesema Kagenzi
Mlinzi huyo ameenda mbali zaidi na kufichua mipango ya kigaidi inayofanywa na Chadema huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.
“Chama ambacho kinandoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia .
"Waliniteka na kunifungia kwenye chumba cha mateso wanachomiliki wao, wamenichoma visu na kuniweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza nitaje wanaonituma. Jamani nawaambia ukweli na watanzania wajue, situmwi na mtu yeyote” .
"Waliniteka na kunifungia kwenye chumba cha mateso wanachomiliki wao, wamenichoma visu na kuniweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza nitaje wanaonituma. Jamani nawaambia ukweli na watanzania wajue, situmwi na mtu yeyote” .
Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho na kusema kuwa mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze nguvu za kiume .
Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa, Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo kwani hata simu yake haina salio na haijawahi kupokea pesa hizo.
Kagenzi amehitimsha kwa kusema kuwa baada ya mahojiano na jeshi la polisi sasa anajipanga kufungua kesi mahakamani ili kuwashitaki CHADEMA kwa mateso waliyompa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro











Post a Comment
Post a Comment