March 19, 2025 09:05:24 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
yanga mashabiki
Ligi kuu Tanzania bara imeendelea jioni ya leo katika viwanja viwili tofauti ambapo kwenye uwanja wa Taifa Dar, Yanga walikuwa wenyeji wa Kagera Sugar huku kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga wenyeji Mgambo JKT waliikaribisha Simba.

Matokeo ya kutoka uwanja wa Taifa Dar, Yanga wamerejea katika usukani wa ligi hiyo na kuishusha Azam iliyokuwa kileleni kwa kufikisha pointi 34 nyuma ya Azam wenye pointi 33 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa.
Yanga walionekana kucheza kwa kujiamini ambapo dakika ya 6 Simon Msuvaanaangushwa ndani ya eneo la hatari ambapo ikaamriwa ipigwe penati ambapo dakika ya 8 Yanga ikapata goli la kwanza kupitia penati.
chereko
Dakika ya 14 Tambwe aliifungia Yanga bao safi la pili baada ya Ngassa kuwazidi mbio mabeki wa Kagera na kupiga cross safi.
Dakika ya 39 Salum Kanoni ameifunga Kagera kwa njia ya penati akimchambua kipaBarthez baada ya Atuplele Green kuangushwa eneo la hatari.
Kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, Simba wanaonja machungu baada ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya maafande wa Mgambo JKT.
Simba ambao walianza kwa kuwakamia zaidi wapinzani wao bahati haikuwa upande wao ambapo dakika ya 45 Ally Nassor anaifungia Mgambo bao la kwanza baada ya kupiga shuti kali huku kipa wa Simba, Ivo Mapunda akiwa amezubaa
Dakika ya 63, kipa Ivo Mapunda amepewa kadi nyekundu na Mgambo wakapata penati baada ya kipa huyo kumuangusha mshambuliaji wa Mgambo ambapo dakika ya 67 Fully Maganga anafunga penati na kuiandikia Mgambo bao la pili.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
18 Mar 2015

Post a Comment

 
Top