Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Majira ya asubuhi ya  leo March 16 kumetokea tukio la moto kwenye bweni la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa kiongozi wa kikosi cha zima moto Kinondoni, Juma Lundawa amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ya moto imetokana na shoti ya umeme kwenye bweni la wasichana (Block B) katika chumba ambacho kinatumiwa kuhifadhi magodoro ya wanafunzi.
Wanafunzi walioshuhudia moto huo wamesema moto ulianza majira ya saa mbili asubuhi huku jitihada za kuuzima moto huo zikiendelea mpaka kikosi cha zimamoto kilipofika kuudhibiti moto huo.
Majeruhi wa tukio hilo ni wanafunzi wawili ambao wamepelekwa katika hospital ya Muhimbili kupata huduma ya matibabu.
Hapa ni picha kutoka eneo hilo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top