Mtoto wa aliyekuwa muimbaji wa R&B marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown amehamishwa kutoka kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Emory alipokuwa amelazwa, na kupelekwa kwenye rehab iliyoko Atlanta, Marekani japo hatua hiyo sio ishara kwamba ameanza kupata nafuu yoyote.

Kwa mujibu wa TMZ, Bobby Kristina alihamishiwa katika rehab hiyo siku ya Alhamisi wiki hii, baada ya madaktari wa hospitali ya Emory kujaribu kwa mara nyingine kumuondolea taratibu mashine ya kumsaidia kupumua ili kuona kama kutakuwa na mabadiliko yoyote. Lakini madaktari wamesema kuwa hakuna nafuu yoyote iliyoonekana na bado yuko kwenye hali aliyokuwa nayo wiki nne zilizopita.
Baba mzazi wa Bobbi Kristina, Bobby Brown bado ana imani kwamba mwanaye atapata fahamu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment