Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MSANII wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koletha’ amewataka mastaa wa kike kuzitumia vizuri fedha wanazohongwa na vigogo kwa kuwekeza kwenye miradi ili ziwanufaishe.

Koletha alisema suala la wasanii wengi wa kike kuishi kwa kutegemea wanaume wakware lipo wazi kabisa, isipokuwa wengi wao wanajisahau kwa kuzitumia hovyo kwa starehe badala ya kuwekeza kwenye miradi.

“Wasanii wengi wanategemea kuhongwa lakini wawe makini na hao wanaowahonga, kama ni gari wapewe kadi na chochote kile kiwe na uthibitisho ili mwisho wa siku wasiumbuke na kuchekwa lakini cha muhimu zaidi ni kuwekeza kwa maisha ya baadaye maana wengi wanaishia kujivunia nyumba za kifahari za kupanga wakati uwezo wa kujenga upo,” alisema Koletha.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top