Tuzo za muziki za Tanzania, Kilimanjaro Music Awards kwa mwaka 2015 zimezinduliwa rasmi.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli akiongea na waandishi wa habari
Uzinduzi huo umefanyika Jumatatu hii kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la LAPF jijini Dar es Salaam.
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA, Godfrey Ngereza
Akiongea na waandishi wa habari, meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli amedai kuwa zoezi la wananchi kupendekeza majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo litaanza March 30 hadi April 19.
Tuzo za mwaka huu zina jumla ya vipengele 34.
Wananchi watapendekeza majina hayo kwa kutumia tovuti, sms na whatsapp.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA, Godfrey Ngereza alisisitiza kuhusu umuhimu wa wasanii kujisali kwenye baraza hili kwakuwa mwakani hakuna msanii atakayehusishwa kwenye zoezi hili kama hatokuwa amejisajili.
Meneja udhamini wa TBL, George Kavishe (kulia) akiongea na waandishi wa habari. Kushoto ni meneja wa Kilimanjaro, Pamela Kikuli
Naye meneja udhamini wa kampuni ya bia, TBL, George Kavishe alisema kuwa kwa mwaka minne sasa kasoro zilizokuwa zikijitokeza kwenye mchakato wa tuzo hizo likiwemo lile la wasanii kujiondoa zimepungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa maboresho mengi yamefanikiwa pamoja na kutolewa elimu kwa wasanii.
Alex Ofio wa Aim Group akionesha namna mbalimbali za wananchi kupendekeza majina kwenye tuzo hizo
Kilele cha tuzo hizo kimepangwa kuwa June 13 mwaka huu.
Source Bongo5
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment