Siku moja baada katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo Mhe Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani ya CCM.
Mhe Lowassa anatoa kauli hiyo katika muendelezo wa kupokea makundi mbalimbali ya jamii kumshawishi kuwania nafasi urais ambapo safari hii waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 60 na wananchi wa kawaida wamefunga safari kutoka wilayani Mbarali mkoa wa Mbeya mpaka mjini Dodoma kumshawishi agombee ambapo amesema kauli ya Nape Nnauye inamshangaza kwani chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kujadili mambo kama hayo kupitia vikao mbalimbali.
Mhe Lowassa pia akawataka wanaoendelea kumnyooshea vidole kuhusu hatua ya wananchi wenye imani naye kujitokeza kumshawishi awanie nafasi hiyo wasubiri ufike wakati muafaka ili wana-CCM na wananchi waweze kutoa maamuzi yao huku akisisitiza watu hasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemuhitaji.
Awali kundi hilo la vijana na bodaboda waliosafiri umbali wa kilometa zaidi ya 600 wakiongozwa na kamanda wa UV-CCM wilaya Mbarali Ibrahim Ismail wamesema lengo la safari yao hiyo ni kuungana na watanzania wengine kumtia moyo Mhe Lowassa ashawishike kuwania urais kwani wana imani kubwa naye huku wakidai pamoja na mambo mengine kama alivyoweza kujenga shule za kata nchi nzima pia ataweza kutegua bomu la tatizo la ajira hasa kwa vijana.
Via>>ITV
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa08 Sep 20160
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama choch...Read more ?
- Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba01 Sep 20160
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananch...Read more ?
- Breaking News: Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho31 Aug 20160
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Opare...Read more ?
- Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana25 Aug 20160
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tu...Read more ?
- Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF23 Aug 20160
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ...Read more ?
- Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi23 Aug 20160
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Maha...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment