Staa wa Bongo Movies, Riyama Ally, amewataka Watanzania kuwa na hofu ya Mungu na kuacha kuwadhulumu uhai wao walemavu wa ngozi ‘albino’.
Akizungumzia swala hilo Riyama alisema inashangaza watu ambao wamekuwa wakiendekeza imani za kishirikina, kwani wengi wao hushia pabaya na kukosa mafanikio.
Alisema imani potofu zimekuwa zikizidisha maovu hayo, huku baadhi ya watu wakijinufaisha wao bila kuangalia maisha ya wenzao.
“Jiulize je mimi na wewe tungezaliwa albino? Vipi na wewe unae fanya ukatili huu ama unatumia watu kufanya kwa tamaa zako za mali na utajiri tungezaliwa albino je tungeweza kupokea adhabu hii ambayo wenzetu ndugu watoto wetu mnawapatia? Tuache mila potofu turudi katika hofu ya Mungu mali utajiri vyeo vyote tutaviacha hapa duniani” Riyama alieleza.
Alisema jamii inapaswa kuamka na kusimama kwa pamoja, kuwatetea albino ili kupunguza vifo na kuwapa maisha ya amani.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment