March 19, 2025 10:51:47 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.
Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.
Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.
Ndege hiyo ya Ujerumani ilianguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.
Hali ya hewa katika eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha kukabiliana na mikasa kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.
Waziri wa Maswala ya ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla ya mawasiliano yake kutoweka .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
24 Mar 2015

Post a Comment

 
Top