Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Diamond Platinumz, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameonekana kuwa karibu na kijana aitwae Sweddy, hali iliyoibua maswali mengi kwa mashabiki wake kuwa huenda ndo mrithi wa Diamond.
Penny akiwa ameshikwa kioni na Sweddy anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa
Penny akiwa ameshikwa kiuno na Sweddy anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa

Baada ya gazeti la Ijumaa march 9 kuandika kuwa Penny amepata mrithi wa Diamond, Bongo5 iliamua kuwatafuta wote wawili Penny na Sweddy na kuzungumza nao kuhusiana na uvumi huo.
DSC003162
Penny ameiambia Bongo5, kuwa karibu na kijana huyo haimaanishi kuwa ni mpenzi wake.
Penny akiwa na Sweddy baada kupigana mabusu
Penny akiwa na Sweddy

“Hahahahaha hah yakawaida haya mabusu,” alisema Penny, sisi ni washikaji, Sweddy namjua toka akiwa mdogo ndo maana unaniona naye kila sehemu,” alimalizia huku alicheka Penny.

Sweddy naye alisema kuwa Penny ni mshikaji wake huku akidai kumpiga mabusu hata hadharani ni kawaida yake na wameshazoea.
“Penny ni mshikaji wangu wa muda sana, mimi nina demu wangu na yeye anajua kila kitu, haya mabusu yakawaida tu, tumeshazoea,” alisema Sweddy huku akicheka.
~Bongo5

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
14 Mar 2015

Post a Comment

 
Top