Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Chelsea
CHELSEA Leo hii Uwanjani Wembley Jijini London wametwaa Taji la kwanza la Msimu, likiwa Kombe la kwanza kwa Meneja wao Jose Mourinho tangu 2012, walipoichapa Tottenham Bao 2-0 katika Fainali ya Kombe la Ligi huko England ambalo sasa linaitwa Capital One Cup.
Kipindi cha Kwanza Tottenham walitawala lakini Chelsea walipata Bao lao la Kwanza Dakika ya 45 kutokana na Frikiki ya Willian kushindwa kuokolewa na Beki wa Spurs Danny Rose ambae Kichwa chake duni kilimfikia John Terry aliepiga Mpira uliomgonga Harry Kane na kumbabaisha Kipa wao Hugo Lloris na kutinga.
Dakika ya 56 Chelsea walipata Bao lao la Pili baada ya Shuti la Diego Costa kumbabatiza Beki wa Spurs Kyle Walker na kumhadaa Kipa Hugo Lloris.
Kwa kutwaa Capital One Cup Chelsea wanahakikishiwa kucheza Ulaya Msimu ujao kwenye UEFA EUROPA LIGI lakini kama watamaliza kwenye 4 Bora za Ligi Kuu England watacheza UEFA CHAMPIONZ LIGI badala yake.
VIKOSI:
Chelsea: Cech; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Cahill, Ramires; Willian, Fabregas, Hazard; Costa
Akiba: Courtois, Filipe Luis, Ake, Oscar, Cuadrado, Drogba, Remy.
Tottenham: Lloris; Walker, Dier, Vertonghen, Rose; Bentaleb, Mason; Chadli, Eriksen, Townsend; Kane
Akiba: Vorm, Davies, Fazio, Dembele, Stambouli, Lamela, Soldado.
REFA: Anthony Taylor

Chelsea captain John Terry lifts the Capital One Cup after leading his side to a comfortable victory over Tottenham at WembleyMourinho lies on the ground as Chelsea celebrate winning the Capital One Cup at Wembley on Sunday
Chelsea tweeted this photograph from inside their dressing room as the players celebrated the 2-0 victory over their London rivalsMourinho walks away behind the stage after Chelsea lift the trophy and are crowned Capital One Cup winnersMourinho joined in as Chelsea celebrated beating Tottenham to lift the Capital One Cup trophy at WembleyDiego Costa, John Terry and Didier Drogba start the celebrations after the final whistle as Chelsea prepare to lift the trophy

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top