BAO la Mrisho Khalfan Ngassa limeipeleka Yanga
SC Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuitoa BDF XI ya
Botswana kwa bao la ugenini. Yanga SC usiku huu imefungwa mabao 2-1 na BDF
Uwanja wa Lobatse na BDF na kufanya isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2,
baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa
mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 30 kwa
kichwa, akimalizia pasi ya Amissi Tambwe ambaye alipokea krosi ya Simon Msuva.
Mrisho Ngassa kwa mara nyingine leo ameonyesha umuhimu wake Yanga SC
Mapema dakika ya 21, BDF walipata pigo baada ya beki wake, Othusitse Mpharitlhe
kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kumfuatia kumchezea rafu winga
wa Yanga SC, Simon Msuva. Kipidi cha pili BDF waikianza vizuri na kufanikiwa
kupata bao la kusawazisha dakika ya 49 kupitia kwa Mosimanyana aliyemalizia
kazi nzui ya Lerole.

Dakika ya 72 mshambuliaji Danny Mrwanda alitolewa nje
baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu beki wa BDF.
BDF walipata bao la pili dakika ya 85 kupitia kwa Kumbulani Madziba aliyewatoka
mabeki wa Yanga kabla ya kumtungua Ally Mustafa ‘Barthez.’ Yanga SC sasa
watamenyana na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimababwe katika
Raundi ya Kwanza.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Barthez, Juma Abdul, Oscar
Joshua, Kevin Yondan, Nadir Cannavaro, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna
Niyonzima, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa/Kpah Sherman dk87.
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment