Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Irene Uwoya amesema ingawa Jaguar alishindwa kuja kuzungumza na wazazi wake kuhusu ndoa yao, bado wanawasiliana vizuri na kila kitu kipo sawa.
10895131_873265689390899_1051658226_n
Akizungumza na Bongo5 leo, Irene amesema mahusiano yake na Jaguar yapo japo hajafanya maamuzi ya kuolewa.
“Jaguar hakuja kuna vitu ambavyo vilitokea vikasababisha asije,” amesema mrembo huyo. “Kila siku naongea naye na uamuzi wake upo pale pale. Mimi mwenyewe bado sijafanya maamuzi ya kusema niolewe lakini akija ndo tutaongea kila kitu.”
Haya hivyo Irene amesema hawezi kuzungumzia ndoa yake na mcheza soka wa Rwanda, Ndikumana waliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Krish.
“Sasa kuhusu hilo nisingependa kuliongelea, mimi nadhani sijui hata nisemeje, sipendi kuongelea mambo yangu binafsi.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
03 Feb 2015

Post a Comment

 
Top