March 20, 2025 11:57:45 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei.
Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa.
Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung.
Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.
Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan.
Mwezi Julai mwaka uliopita watu 48 walikufa baada ya ndege ya shirika hilo la TransAsia kupata ajali kutokana na hali mbaya ya hewa katika kisiwa cha Penghu. bonyeza hapa kuangalia video

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
04 Feb 2015

Post a Comment

 
Top