March 16, 2025 07:44:30 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
HANDCUFFS (1)
Jamaa mmoja huko Taiwan mama yake alikuwa anaumwa, baada ya kutbiwa Hospitali alirudishwa nyumbani kwa mapumziko lakini mtoto wake wa kike hakuonekana kujali hali hiyo ya mama yake, alikuwa akimsumbua mama huyo mara kwa mara kudai hela kitu ambacho kaka yake hakupendezwa nacho.

Kaka huyo ambaye anaitwa Wang aliamua kumchoma kisu dada yake kutokana na kutopendezwa na usumbufu anaofanyiwa mama yake huo, ambapo dada huyo alifariki.
Wang muda mwingi hukaa nyumbani kumhudumia mama yake na kufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo kupika na kufanya usafi lakini dada yake hakuwa msaada wowote kwa mama yake, ni mtu wa kushinda na rafiki zake.
Baada ya kufanya mauaji hayo alishafisha eneo hilo, akamuandalia mama yake breakfast na chakula cha mchana, baada ya mama yake kupumzika Wang aliwaita Polisi na kukiri kuhusika na tukio hilo kutokana na kuchoshwa na matatizo ya nyumbani kwao na kudai kuwa  dada yake mara nyingi amekuwa akimuonea mama yao ikiwemo kumdai fedha kila siku na kwenda kutumia na rafiki zake.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
02 Feb 2015

Post a Comment

 
Top