Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


BAADA ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kutofunga vizuri vifungo vya suti yake, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira ameamua kumuona mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ili aanze kumtengenezea suti zake.

Mhe. Wasira ameamua kukutana na mbunifu huyo aliyeanza mara moja kumchukua vipimo vyake ili amtengenezee mavazi yake ambayo atakuwa akiyatumia katika shughuli zake mbalimbali za kiserikali.


Picha za Waziri Wasira zilienea mitandaoni alipopiga picha ya pamoja akiwa na Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.

Kwa kuamua kumuona Sheria Ngowi, Mhe. Wasira atakuwa amepata mti shamba wa tatizo hilo lililotawala mitandao ya kijamii hivi karibuni.

 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
12 Feb 2015

Post a Comment

 
Top