Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Jamuhuri na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa kuteketea. kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Jamuhuri na moski.
Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Source:Michuzijr
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro












Post a Comment
Post a Comment