Home
»
Kitaifa
» Mchumi wa Wizara ya Ardhi Afikishwa Mahakamani akituhumiwa Kumshika Matiti Mwanamke bila Ridhaa Yake
MCHUMI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Brown Kajange (42) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo kujibu mashitaka mawili, likiwamo la shambulio la aibu kwa kumshika matiti mwanamke bila ridhaa yake.
Karani wa Mahakama hiyo, Blanka Shao alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Matrona Luanda kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 16, mwaka huu katika eneo la kuuzia samaki la Feri Kivukoni wilaya ya Ilala.
Shao alidai siku ya tukio saa 6 mchana katika eneo hilo, mshtakiwa alimshika matiti Queensia Fusi bila ridhaa yake huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Alidai kuwa shtaka la pili, mshtakiwa alimpiga ngumi mlalamikaji katika jicho la kushoto na kusababisha maumivu makali katika sehemu hiyo. Mshtakiwa alikana mashtaka na Hakimu Luanda aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 3, mwaka huu itakapotajwa.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka serikali ya mtaa, atakayesaini bondi ya Sh 300,000.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 9 201609 Sep 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September 09 201...Read more ?
- Viongozi wa Afrika Mashariki Waigomea Ulaya....Wajipa Miezi Mitatu Kuutafakari Mkataba wa EPA09 Sep 20160
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa miezi mitatu kuju...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa Leo Bungeni kuhusu wahusika wa mauaji ya askari08 Sep 20160
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na ...Read more ?
- Makamu wa Rais: Viongozi Na Watumishi Wa Umma Kuchukuliwa Hatua Kali Iwapo Watabainika Kukiuka Taratibu Za Kazi08 Sep 20160
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya M...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment