Mtoto wa kike wa marehemu, Whitney Houston, Bobbi Kristina yupo mahututi na ubongo wake umedaiwa kushindwa kufanya kazi. Madaktari wamedai kuwa hiyo si dalili nzuri.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 alikutwa bafuni kwenye ‘bathtub’ uso wake ukiwa kwenye maji Jumamosi iliyopita na alikuwa hapumui.
Alizinduka na kupelekwa hospitali ambako amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi ambako amewekwa kwenye coma. Pia amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua lakini vipimo vinaonesha kuwa hali ya ubongo wake ipo chini mno.
Baba yake na Bobbi Kristina, Bobby Brown, yupo pembeni ya kitanda alicholazwa mwanae.
Madaktari wameiambia familia yake kuwa iendelee kusali na kuwa na matumaini japo dalili si nzuri.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment