March 21, 2025 10:28:26 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

waasi wa houthi wakiuzunguka mji mkuu wa yemen Sanaa
Mgogoro nchini Yemen umechukua mkondo mwengine alhamisi baada ya ripoti za maafisa kusema kuwa Rais na waziri mkuu pamoja na serikali yao wamejiuzulu.Hatua hiyo inajiri baada ya serikali hiyo kutoa ombi la kujiuzulu huku kukiwa na sitofahamu kati yake na waasi wa Houthi maafisa wamesema.
Serikali hiyo ilibuniwa mnamo mwezi Novemba kufuatia makubaliano yalioafikiwa na umoja wa mataifa.
Wapiganaji wa Houthi bado wanaendelea kudhibiti mji mkuu wa sanaa mbali na kumteka msadizi mmoja wa rais wiki iliopita.
Walikuwa wamekubali kuondoka katika maeneo muhimu katika kasri ya ikulu ya rais na nyumba ya rais Abdrabbuh Mansour Hadi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
22 Jan 2015

Post a Comment

 
Top