Na Mayasa Mariwata/UWAZI
MSANII wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, Ruta Maximilian Bushoke wamemwagana na hakuna cha ndoa tena.
Akizungumza na Uwazi, Kabula alitoa ya rohoni na kusema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mwenzake haoneshi msimamo katika mkakati wao wa kuoana hivyo kwa sasa wamebaki kuwa marafiki wa kawaida tu kwa sababu wote ni wasanii.
“Tumeshaachana, mwaka huu nimeuanza kwa kuwa bize na mambo yangu mengine ya kikazi siyo mapenzi tena. Tulikuwa tumepanga vizuri kwamba tutaoana na kuamini hivyo kwa kipindi chote alichokuwa nchini Afrika Kusini.”
“Baada ya mwenzangu kutua Bongo, hakuonesha dalili yoyote ya kutekeleza hilo suala la ndoa. Sikuwa na uwezo wa kusema nimfunge kamba ndiyo nimlazimishe kumpeleka kwetu tuoane, nimeona bora niachane naye kwani nimeshachoka na maisha ya uzinifu nahitaji kuingia katika ndoa,” alisema Kabula.
Bushoke alipotafutwa kwenye simu hakupatikana lakini kwa mujibu wa marafiki zake wa karibu wanasema kuwa amesharudi Afrika Kusini.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Mapenzi Yamtokea PUANI Davina24 Jul 20150
Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya amedaiwa kutoswa na mwanaume aliyemuachanisha na mumewe...Read more ?
- Kigogo Mpya Wa Jack Wolper Anaswa02 May 20150
Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibong...Read more ?
- Vanessa Mdee: Japo Nina Boyfriend (Jux) ila Sasa Hivi Siwezi Kuwa na Mtoto…Ifahamu Sababu26 Apr 20150
Muimbaji wa ‘Nobody But Me’ Vanessa Mdee a.k.a Vee Money ambaye hivi sasa ameweka wazi uhusiano w...Read more ?
- Naima wa Aslay Ndani ya Penzi Zito na Kipa wa Simba Manyika JR ..Adaiwa Kumshusha Kiwango cha Mpira Awapo Uwanjani21 Apr 20150
Baada ya kuwapa majibu wale wote ambao waliokua wanadai kwamba ameshuka kiwango, hivi sasa watu ...Read more ?
- Mahaba Niue! Siri ya Mapenzi Yao Iko Moyoni Mwao Wenyewe17 Apr 20150
Mastaa wengi wamekuwa wakiingia kwenye uhusiano na kufanya siri kubwa. Wapo ambao wanaonekana dhah...Read more ?
- Hatimaye Shamsa Ford Atoboa Kuwa Nay ndio “EndlessLove” Wake14 Apr 20150
Staa mrembo wa Bongo Movies Shamsa Ford ambae siku za hivi karibuni alikanusha waziwazi alipoku...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment