Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Washambuliaji, Emmanuel Okwi wa Simba SC (kushoto) na Kipre Tchetche wa Azam FC (kulia) wakipambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Januari 25,2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

 Timu hizo zilitoka sare ya 1-1, bao la Simba SC akifunga Okwi kipindi cha kwanza na la Azam FC Kipre Tchetche kipindi cha pili. 

Huko Mjini Mbeya, Uwanja wa Sokoine, Dabi ya Jiji hilo ilimalizika kwa Sare ya Bao 2-2 wakati Mbeya City ilipovaana na Tanzania Prisons.

Nao Mtibwa Sugar, ambao walikuwa hawajaonja kipigo Msimu huu kwenye Ligi, Leo hii Januari 25,2015 wamechapwa 2-1 Ugenini na Ruvu Shooting.

Matokeo haya ya Leo yamewabakisha Azam FC kileleni mwa Msimamo wa Ligi wakiwa na alama 21 kwa Mechi 11 wakifuatiwa naYanga SC wenye alama 18 kwa Mechi 10 na kisha Mtibwa Sugarwenye Pointi 17 kwa Mechi 10 pia  huku Simba SC ikiwa na alama 13.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 Jan 2015

Post a Comment

 
Top